Nelson K. Tunoi Mwandishi Msaidizi wa Sheria, Kenya Law Baraza la Kitaifa la Kuripoti Sheria (kwa jina la kimaarufu Kenya Law) linatambua matumainio ya wakenya kuwa na serikali ambayo ina maadili ya kuzingatia haki za kibinaadam, usawa, uhuru, demokrasia, haki ya wananchi na kuzingatiwa kwa sheria. Kufuatia haya, Kenya Law imejitambulisha kama kituo kinachoongoza katika kuwezesha raia kupata habari au nakala rasmi za kisheria zinazoeleweka, kwa wakati unaofaa na katika mifumo ambayo inawajumuisha raia wote . Kama kitengo cha utafiti wa kisheria, Kenya Law inawajibika kikatiba kuhakikisha ya kwamba haki ya raia ya kupata habari rasmi za kisheria inatekelezwa. Kwa kutekeleza wajibu huo, Kenya Law inachangia katika ustawi wa jamii na utawala bora wa kisheria kupitia kupatikana kwa urahisi kwa sheria na kuelewa kwa kina sheria za bunge, maamuzi ya mahakama na mandhari za kisheria zinazohusiana na wananchi katika nyanja mbali mbali za maisha yao. Kufuatia haya Kenya Law, ikishirikiana na Languages Africa, imeanzisha mpango wa kutafsiri muhtasari wa nakala rasmi za kisheria, ikianza na maamuzi ya mahakama, kutoka lugha ya Kiingereza hadi lugha ya Kiswahili ambayo kwa mujibu wa katiba ni lugha rasmi ya kitaifa. Mojawapo ya changamoto tunayokabiliana nayo katika mpango huu ni kupata tafsiri mwafaka ya maneno, mandhari na misemo sugu ya kisheria. Ili kurahisisha kazi yetu, tungependa kujumuisha raia katika kuchangia kazi ya utafsiri. Ifuatayo ni orodha ya maneno, mandhari na misemo sugu ya kisheria na tafsiri yetu. Tungependa kujua kutoka kwako ikiwa tafsiri yetu ni kamili. Kuchangia kwako kutasaidia kutukuza lugha ya taifa na pia kueleweka kwa sheria na raia wote wa Kenya. Katika jaribio au pendekezo lako la kutafsiri, tafadhali zingatia umuhimu wa kujiepusha na misamiati sugu ya Kiswahili na badala yake tumia lugha nyepesi inayowasilisha maana ya maneno au misemo inayotafsiriwa. Jumuika nasi na uchangie kwa kujisajili katika mtandao huu au kunukuu maoni yako chini ya ukurasa huu. English Version: Kenya Law recognizes the aspirations of Kenyans for a government based on the essential values of human rights, equality, freedom, democracy, social justice and the rule of law. Pursuant to this, Kenya Law has established itself as a leading legal resource centre by ensuring that it provides credible, comprehensible and timely legal information that is open and accessible to all. As a leading legal resource frontier, Kenya Law is constitutionally obligated to ensure that the right to access to legal information is guaranteed, hence serving the greater needs of society and good governance through easy access to laws of Kenya, judicial opinions and other pertinent issues of public interest. Pursuant to this, Kenya Law in collaboration with Languages Africa, has commenced the exercise of translating the case summaries of judicial opinions, from English to Swahili, which is the national language as stipulated in the Constitution. One of the major challenges we are facing in this exercise is to establish the standard translation of legal words and phrases. We would like to involve the public to participate in this exercise so as come up with an acceptable and standardized glossary of legal terms. The glossary below contains some of the English-Swahili legal words, terms and phrases already compiled. We would like to get your views on whether our translations of these words are correct. Your involvement and participation would assist in embracing our national language and help in promoting the knowledge of law to all citizens of Kenya. In your attempt or interest to translate, please avoid as much as possible complex phrases and instead substitute them with easy Swahili phrases or words that clearly express the meaning of the words, terms or phrases being translated. Join us and contribute in developing our glossary of English-Swahili terms by registering and submitting your comments on this page.
KAMUSI YA MANENO NA MISEMO YA KISHERIA
English Swahili
1 Abbreviations Ufupisho
2 Absorption Maingizi
3 Accordance Ulinganifu
4 Accountability Uajibikaji
5 Accountable Uajibikaji
6 Accredited Patiwa Kibali/Idhinishwa
7 Acknowledging Kubali/Kumbatia
8 Acquiesced Kukubali
9 Acronyms Akronimu
10 Act Kifungu cha Sheria
11 Adequate Toshelevu
12 Adherence Utiliaji maanani
13 Adopt Chukulia
14 Advancement Uchukuaji wa hatua/Maendeleo
15 Adverts Matangazo
16 Advocate Kutetea
17 Agenda Ajenda
18 Aligned Pangiliwa
19 Alignment Upangiliaji
20 Allegations Madai
21 Allege Dai
22 Alliances Miungano
23 Allocation Ugavi
24 Altruism Ubinadamu/Uungwana/Utu
25 Analysis Uchanganuzi
26 Anchored Kita mizizi
27 Anchoring Ukitaji mizizi
28 Annulling Kutupilia mbali
29 Anomaly Jambo lisilo la kawaida
30 Anticipate Tarajia
31 Anticipation Matarajio
32 Appeal Kata rufaa
33 Appellant Mkataa Rufaa/Anayekata Rufaa
34 Application Matumizi
35 Appoint Teua
36 Appraisal Ukadiriaji wa Ubora wa kazi
37 Approach Mtazamo
38 Approaches Mitazamo
39 Appropriate Mwafaka/Yenye kufaa
40 Argument Hoja
41 Arisen Iliyotokeya
42 Aspirations Maazimio
43 Attorney General Mwanasheria Mkuu
44 Automated Fanywa otomatiki
45 Backlog Limbikizo
46 Benchmarks Vilengwa
47 Bill Mswada
48 Bill of Rights Sheria ya Haki za Binadamu
49 Blueprint Mwongozo/Mpango Makini
50 Bold Kolevu
51 Brand Identity Utambulisho wa Nembo
52 Branding Uwekaji nembo
53 Budgetary Allocation Ugavi wa Bajeti
54 Burden of proof Wajibu wa kuthibitisha ushahidi/Jukumu la kutoa ushahidi
55 Bureaucracy Urasimu
56 Bureaucrat Mrasimu
57 Business Models Miundo ya Biashara
58 By Virtue Kwa mujibu wa
59 Capita Kila mtu/Mwananchi
60 Captured Wekwa/Chukuliwa
61 Career Ajira
62 CD-ROM SANTURI
63 Character Sifa bainifu
64 Chart Chati/Mchoro
65 Chief Justice Jaji Mkuu
66 Chiefly Haswa
67 Circulars Barua
68 Civil Case Kesi ya Madai
69 Civilized Yenye ustarabu
70 Cognizant Mjuzi/Mwenye Ujuzi
71 Collaboration Ushirikiano
72 Collaborative Mechanisms Mifumo ya Ushirikiano
73 Commercial Purposes Makusudio ya Biashara
74 Commitment Kujitolea
75 Competitive Yenye upinzani
76 Compliance Ukubalifu
77 Compliant Kubalifu
78 Comply Zingatia
79 Components Vipengele/Viungo
80 Condemn Shutumu/Laani
81 Conducive Inayofaa
82 Conferred Shauriana/Jadiliana
83 Conformity Ukubalifu
84 Consolidate Weka pamoja
85 Constitution Katiba
86 Constraints Vizuizi
87 Consultation Ushauriano
88 Consumers Watumizi/Watumiaji
89 Contest (a seat) Gombea
90 Contest (challenge) Pinga/Kataa
91 Conventions Mikataba/Makongamano
92 Co-ordination Uratibu
93 Core Functions Kazi Kuu
94 Core Values Maadili Makuu
95 Corruption Ufisadi
96 Court of Appeal Mahakama ya Rufaa
97 Creditor Mkopeshaji
98 Crisis Mgogoro/Upeo wa matatizo
99 Critical Muhimu
100 Critique Kupinga/Changamoto
101 Curator Mtunza/Mwangalizi
102 Curricula Mitaala
103 Curriculum Mtaala
104 Custodian Mwangalizi
105 Day-to-Day Siku-baada-ya Siku
106 Dean Mkuu
107 Debt Deni
108 Debtor Mdai/Mkopaji
109 Debtors’ issue Swala la mdaiwa
110 Defendant/Respondent Mshtakiwa
111 Define Fasili/Fafanua
112 Dictate Kariri
113 Directorate Bodi ya Wakurugenzi/Ukurugenzi
114 Disabilities Ulemavu
115 Discourse Hotuba/Mjadala
116 Discrepancies Hitilafu/Tofauti
117 Disputable Yenye uwezo wa kuleta ubishi/Mzozo
118 Disputant Mbishi/Mzushaji
119 Dispute (noun) Ubishi/Mzozo
120 Dispute (verb) Bishana/Zozana
121 Disseminate Kueneza
122 Distribute Kugawa
123 Donor Conditionality Masharti ya Mfadhili
124 Elaborately Vizuri
125 Elect Chagua
126 Election petition Kesi ya kupinga uchaguzi
127 Elements Elementi
128 Emerge Ibuka
129 Emerging Inayojitokeza
130 Enabler Kiwezeshaji
131 Enact Tunga
132 Engage Husisha
133 Enhanced Boreshwa
134 Enlightened Ufahamu
135 Enlightened Society Jumuia Iliyofahamishwa
136 Essence Umuhimu
137 Ethics Maadili
138 Evidential burden Ushahidi wa kuthibitisha
139 Evolved Kengeushwa
140 Excellence Ubora
141 Exceptions Mambo ya kipekee/Yasiyo ya kawaida
142 Executive Watoaji uamuzi
143 Executive Arm Tawi la Utoaji Uamuzi
144 Exemplary Performance Utendakazi wa kupigiwa mfano
145 Expectations Matarajio
146 Expedite Kuharakisha
147 Explicitly Waziwazi
148 Feedback Majibu
149 File (verb) Andikisha/Sajili
150 Financial Resources Rasilimali za Kifedha
151 Flag out Alamu
152 Flawed Pungufu/Yenye Makosa
153 Focus Lengo
154 For a Mabaraza
155 Forge Songa mbele
156 Formats Maumbizo
157 Foster Imarisha
158 Fostering Kuendeleza
159 Fountain Chemichemi
160 Framework Mpangilio
161 Fraud Udanganifu/Ulaghai
162 Freezing Of Funds Ufichwaji wa Fedha
163 Fulfillment Utimizo
164 Fundamental Restructuring Upangaji upya Muhimu
165 Future Siku za usoni
166 Gender-Based Unaohusiana na Jinsia
167 General Public Umma wa Kawaida
168 Generate Zalisha
169 Globally Kilimwengu/Ulimwenguni kote
170 Goodwill Usaidizi
171 Governance Utawala
172 Grant Msaada
173 Harmonization Upatanifu
174 Harnessing Kuimarisha
175 Heads Of Department Wasimamizi wa Idara
176 Heritage Urithi
177 Human Resource Wafanyikazi
178 Impacted Athirika
179 Impropriety Utovu wa nidhamu
180 In light of Kwa mujibu wa
181 In this regard Kwa mujibu wa
182 In View of Kwa mujibu wa
183 Inadequate Isiyotosha
184 Inaugural Uzinduzi
185 Incentives Motisha/Ushawishi
186 Incorporated Uhusishwaji
187 Indicators Vionyeshi
188 Indigenous Asilia
189 Industrializing Uundaji viwanda
190 Inflation Mfumuko wa bei
191 Infrastructural Miundomsingi
192 Innovation Ugunduzi
193 Innovative Ugunduzi
194 Inspired Hemshwa
195 Instituted Iliyowekwa pamoja
196 Institutions Taasisi
197 Integrated Monitoring Ufuatilizi Tangamani
198 Integrity Uadilifu
199 Interactive Tangamani
200 Interdepartmental Mawasiliano kati ya Idara
201 Interim Committee Kamati ya Muda
202 Internship Uanagenzi
203 Invalid Batili/Haramu
204 Invalidate Batilisha/Fanya kuwa Haramu
205 Invalidation Ubatili/Uharamishaji
206 Invalidity Batilisha/ Hali ya kufanya kuwa haramu
207 Inventory Orodha/Hesabu
208 Irregularities Mambo yasiyofuata kanuni
209 Journal Jarida
210 Judge Jaji
211 Judiciary Affairs Maswala ya Idara ya Mahakama
212 Jurisdiction Mamlaka ya kisheria
213 Jurisprudence Falsafa/Taaluma ya sheria
214 Knowledge Maarifa
215 Law Sheria
216 Leadership Uongozi
217 Leave of Court Idhini ya Mahakama
218 Legal burden Wajibu wa kisheria
219 Legal Notice Arifa ya Kisheria
220 Legal regime Mfumo wa kutawala wa kisheria
221 Legislations Sheria
222 Legislature Waundaji sheria
223 Leverage Faidika/Jiinua
224 Liaise Shirikiana
225 Library Maktaba
226 Limited Infrastructure Miundo msingi Finyu
227 Link Kiungo
228 Linkage Uhusiano
229 Linkages Viungo
230 Literacy Elimu
231 Literature Fasihi
232 Litigant Mdai/Mlalamishi
233 Litigation Hatua ya kisheria/Madai mahakamani
234 Livelihoods Hali ya Maisha
235 Lobbying Uhamasishwaji
236 Magistrate Hakimu
237 Mail System Mfumo wa Barua
238 Malpractices Mwenendo mbaya/ Kuzembea kazini
239 Mandate Jukumu
240 Matrix Matriksi
241 Mechanisms Mipangilio
242 Medical Scheme Mpangilio wa Kimatibabu
243 Memorandum Of Understanding Mkataba wa Makubaliano
244 Merely Kuchukuliwa juujuu
245 Milestone Lengo/Fanikio
246 Milestones Mafanikio
247 Mission Mwito
248 Mitigate Punguza
249 Mobilization Uhamasishwaji
250 Monitor Fuatilia
251 Monitoring Ufuatilizi
252 Monitoring, Evaluation And Reporting Ufuatilizi, Utathmini Na Upigaji ripoti
253 Monopoly Ukiritimba
254 Monthlies Kila mwezi
255 Moot Bandia
256 Mutual Pamoja/Pande zote
257 Naught Bure/Dharau/Ambulia patupu
258 Non-Executive Members Wanachama Waso-Watoaji Uamuzi
259 Obligation Jukumu
260 Obsolescence Hali ya kupitwa na wakati
261 Openness Uwazi
262 Order Amri
263 Organizational Structure Mpangilio wa Shirika
264 Outcomes Matokeo
265 Outlined Ainishwa
266 Outreach Ufikivu
267 Paradigm Dhana/Mfumo
268 Parliamentary Seat Kiti cha Ubunge
269 Partner Mbia
270 Partnership Ushirika/Ubia
271 Path Njia
272 Patriotic Kizalendo
273 Pension Scheme Mpangilio wa Pesa za uzeeni
274 Performance Contracting Utendakazi wa Kandarasi
275 Petition Kesi
276 Petitioner Mlalamishi
277 Philosophical Kifilosofia
278 Pillars Nguzo/Mhimili
279 Plaintiff/Petitioner Mlalamishi
280 Plead Tetea hoja
281 Pleadings Utetezi wa hoja
282 Pocket Size Inayobebeka Mfukoni
283 Policy Sera
284 Political Climate Hali ya kisiasa ilivyo
285 Political Interference uhitilafianaji wa kisiasa
286 Politics Kisiasa
287 Pollution Uchafuzi
288 Popular Version Toleo Maarufu
289 Preceding Kabla ya/Iliyotangulia
290 Premium Teule
291 Prescribe Shauri
292 Presidential Election Petition Kesi ya Uchaguzi wa Kirais/ Kesi ya Kupinga Uchaguzi wa Rais
293 Pre-trial conference Kikao cha kabla ya kesi kuanza kusikizwa
294 Principles Kanuni
295 Prisoner Mahabusu
296 Proceedings Taratibu
297 Procurement Ununuzi
298 Professionalism Utaalamu
299 Progressive Endelevu
300 Projected Sources Asili/Vyanzo Tabiriwa
301 Promise Ahadi
302 Promulgation Uzinduzi Rasmi
303 Proposals Mapendekezo
304 Propriety/Decorum Usahihi/Utaratibu
305 Prosecute Shtaki
306 Prosecuting Offenders Kushtaki Wakiukaji sheria
307 Prosecutor Kiongozi wa Mashtaka
308 Prosperous Yenye mafanikio
309 Provisions Matoleo
310 Prudent Busara
311 Public Umma
312 Publications Machapisho
313 Pupillage Uanagenzi
314 Quality Assurance Uhakiki wa Ubora
315 Quality Control Udhibiti wa Ubora
316 Quality Statement Kauli ya Ubora
317 Queries Maulizio
318 Raft Msururu
319 Ratified Kuridhiwa/Wekwa katika msururu
320 Rationale Maelezo
321 Re-Aligned Pangwa- Upya
322 Reconfigure Badilisha upya
323 Recusal Kujiondoa kwa Jaji
324 Rededicated Kujitolea upya
325 Re-Engineered Kukarabati upya/Kuundwa upya
326 Reforms Marekebisho
327 Refugees Wakimbizi
328 Regional Integration Utangamano wa Kimaeneo
329 Regional Policy Sera ya Kimaeneo
330 Regulation Utaratibu
331 Reinvigorate Kuimarisha
332 Reliability Utegemevu
333 Renewed Mpya
334 Repeal Batilisha
335 Reporting Upigaji ripoti
336 Repositioning Kujipanga upya
337 Repository Hifadhi/Ghala
338 Representation Uwakilishi
339 Research Utafiti
340 Resource Rasilimali
341 Respondent Mshatikwa
342 Revamping Ufufuaji/Uinuaji
343 Revise Durusu
344 Revision Durusu
345 Roadmap Njia kuu
346 Robust Thabiti/Shupavu
347 Rule Sharti
348 Rule of Law Utawala wa Kisheria
349 Schedule Utaratibu/Ratiba
350 Scheme Mpangilio
351 Scorecard Kadimatokeo
352 Secretariat Bodi ya Wakurugenzi/Ukurugenzi
353 Semi-Autonomous Uhuru Kiasi/Uhuru-nusu
354 Sensitizing Kuhamasisha
355 Shared Value Wajibu wetu katika jamii na mazingira
356 Significant Effect Athari Kubwa
357 Significantly Pakubwa
358 Slogan Kaulimbiu
359 Spirit Hali
360 Stakeholders Washikadau
361 Standard of evidence Kiwango cha ushawishi wa ushahidi
362 State Corporation Shirika la Serikali
363 Statute Sheria
364 Statutes Sheria
365 Strategic Plan Mpango wa Mikakati
366 Strategic Themes Maudhui Kazi/Maudhui ya Mikakati
367 Streamlining Upangiliaji
368 Succession Kupokezana kwa Wafanyikazi
369 Taxation Ulipaji ushuru
370 Technical Assistance Msaada wa Kiufundi
371 Technological Kiteknolojia
372 The Judiciary Idara ya Mahakama
373 Threshold Kiwango cha juu
374 Timelines Vipimo vya muda
375 Timely Kwa muda ufaao
376 Titles Vyeo
377 Transform Badilisha
378 Transitional Government Serikali ya Mpito
379 Transmitted Kuenezwa
380 Transparency Unyofu
381 Treaties Mikataba
382 Treaties Database Hifadhidata ya Mikataba
383 Tribunal Baraza la kutoa hukumu/Tume
384 Undermine Dhoofisha/Dhalilisha
385 Underpin Kuimarisha
386 Undertaken Fanywa
387 Unique Point-In-Time functionality Utendakazi wa Hapo-Kwa-Hapo
388 Universal Kilimwengu
389 Uphold Endeleza
390 Usurp Nyang'anya/Pokonya
391 Utilization Matumizi
392 Valid Halali
393 Validate Halalisha
394 Validity Uhalali
395 Values Maadili
396 Vision Maono
397 Web-Based Unaotokana na Wavuti
398 Website Tovuti
399 Wellbeing Wema